Jeremiah 30:12-15

12 a“Hili ndilo asemalo Bwana: “ ‘Kidonda chako hakina dawa,
jeraha lako haliponyeki.

13 bHakuna yeyote wa kukutetea shauri lako,
hakuna dawa ya kidonda chako,
wewe hutapona.

14 cWale walioungana nawe wote wamekusahau,
hawajali chochote kukuhusu wewe.
Nimekupiga kama vile adui angelifanya,
na kukuadhibu kama vile mtu mkatili angelifanya,
kwa sababu hatia yako ni kubwa mno
na dhambi zako ni nyingi sana.

15 dKwa nini unalia kwa ajili ya jeraha lako,
yale maumivu yako yasiyoponyeka?
Kwa sababu ya uovu wako mkubwa na dhambi zako nyingi
nimekufanyia mambo haya.

Copyright information for SwhKC